Utangulizi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina jukumu la kusimamia na kukusanya kodi ya majengo kuanzia Julai 1, 2016 kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya utozaji Kodi ya Majengo Sura 289, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura 290 na
Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Sura 399. Hii imeainishwa kwenye Sheria Fedha ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 na Mabadiliko ya Sheria mbalimbali (The Written laws (Miscellaneous) Amendments Act No. 2 Februari, 2019.

TRA: Taarifa kuhusu kodi ya pango

Kodi ya pango

TRA wametoa taarifa kuhusiana na utoaji wa kodi ya pango inayotokana na mapato ya nyumba kwa asilimia 10%.

TRA ni shirika linalohusika na mapato, na mapato hayo yanatumika katika kufanya maendeleo katika jamii

Mwenye nyumba atapata cheti cha kodi ya zuio kama ushahidi wa malipo ya kodi kutokana na zuio la asilimia 10%